Raia wa Marekani aitwaye Angela Deem ametangaza kutoa kiasi cha dola 10,000 ambayo ni sawa na Tsh/= 25,450,000.55 kwa atakayefanisha kupatikana mumwe aitwaye Michael Ilesanmi, raia wa Nigeria. Aliyepotea kwa takribani miezi miwili tangu ahamie Marekani kwa mkewe.
Angela ametoa kilio hicho na ahadi hiyo ya pesa katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram akiwa LIVE .
Wawili hao wamekuwa pamoja kwa miaka miwili tangu wakutane kwenye kipindi cha mahusiano cha Mchumba wa Siku 90 (90 Day Fiancé,).
Michael alipata umaarufu baada kuwa na mahusiano na mwanamke mkubwa kiumri kutoka nchini Marekani, na Uhusiano wao ulitabiri kuwa hawatadumu.