Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Logos Olori ndio mwandishi wa ‘Unavailable’ ya Davido

Kutoka lebo ya DMW, Logos Olori, amedai kuwa yeye ndio aliyeandika wimbo bosi wake Davido ngoma ya ‘Unavailable’ ambayo alimshirikisha Musa Keys na ngoma hiyo ilitajwa kuwania tuzo ya Grammy 2024.

Lagos amefunguka kuchora ngoma hiyo kupitia mahojiano aliyofanya na Cool FM, ambapo anasema Bosi wake alitaka kitu tofauti hivyo akaona isiwe kesi akatisha kwa staili hiyo.

“Peruzzi aliandika aya hiyo. Baada ya kutengeneza wimbo huo, Davido alisema anataka verse ibadilishwe, akampigia simu Peruzzi ili afanye verse. Lakini kwa kweli nilikuja na wazo la wimbo huo. Tulifanya kidogo ya tweaking; hapo ndipo Musa Keys na Peruzzi waliingia,” amesema Lagos.

Unvailable ni ngoma unayopatikana katika albamu ya Davido ya Timeless iliyotoka Machi, 2023, ikiwa na ngoma zipatazo 17.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *