Rapa Mkongwe na Mfanyabiashara Diddy amefunguliwa mastaka mapya na Unyanyasaji wa kingono na Mtayarishaji wake wa muizki aitwaye Rodney “Lil Rod” Jones
Mbali na unyanyasaji huo pia Lil Rod amefungua kesi ya kudhulumiwa malipo ya uandaaji Albamu ya ‘The Love Album: Off the Grid’.
Kwenye shauri hilo ambalo limefunguliwa kwenye Mahakama ya mjini New York, Rodney amemtuhumu Diddy kwa kumshika shika kimahaba na kwa lengo la kumtaka kingono na pia alilazimishwa kufanyia kazi bafuni wakati Sean “Diddy” Combs akioga na kutembea akiwa mtupu.
Kwa mujibu wa Mahakama, Rodney anadai kiasi cha ($30 million) zaidi ya TSh. BILIONI 76.5 kama fidia. Mtayarishaji huyo anatajwa kuhusika kutengeneza nyimbo 9 kwenye Album ya Diddy “Love” iliyotoka Septemba mwaka 2023.