VIDEO: Polisi Simiyu wafanya ukaguzi wa mabasi

Jeshi la polisi mkoani Simiyu limefanya ukaguzi wa magari ya abiria yanayofanya safari zake mikoani na katika wilaya mbalimbali za mkoa huo, ili kuhakikisha sheria, taratibu na kanuni za usalama barabarani zinafuatwa.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo la ukaguzi lililofanyika leo katika stand ya mabasi ya mkoa wa Simiyu, kamanda wa polisi wa mkoa huo Acp Edith Swebe ameeleza namna ambavyo zoezi la ukaguzi wa magari linavyosaidia katika kuzuia ajali za barabarani.

Nicholas Kamuzola ni afisa mfawidhi wa mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini (LATRA)mkoa wa Simiyu amekemea tabia ya baadhi ya wasafirishaji kuchanganya abiria na mifugo.

Nao baadhi ya abiria wakaeleza namna ambavyo ukaguzi huouna umuhimu na kusema kuwa unawasaidia kupata elimu ya usalama barabarani pamoja kuwaondolea uonevu kutoka kwa wasafirishaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *