Klabu ya Simba SC imetangaza kuwasimamisha wachezaji Nassor Kapama na Clatous Chota Chama kutokana na vitendo vya utovu wa nidhamu.
Taarifa kwa umma ya Wekundu hao wa Msimbazi imebainisha kuwa wachezaji hao watapelekwa katika kamati ya nidhamu kwa hatua zaidi za kinidhamu kufuatia vitendo hivyo
“Uongozi wa klabu ya Simba unapenda kuwakumbusha watumishi wake wote kuzingatia misingi ya maadili na nidhamu kwani klabu haitasita kumchukulia hatua yeyote atakaethibitika kwenda kinyume na utaratibu huo.” imesema taarifa hiyo.