Umewahi kujiuliza Tems na Wizkid walikutana vipi na kutengeneza ngoma la kwenda la ‘Essence’? katika mahojiano aliyofanya na kituo cha radio cha Hot 97 Marekani, Tems anafunguka kuwa EP yake ya kwanza ndio ilichora ramani nzima, hasa ngoma ‘Try Me’.
Mrembo huyo amesimulia kuwa sio mashabiki pekee waliovutiwa na uwezo wake wa sauti na ujuzi kwenye wimbo huo; kwani hata Wizkid alitekwa kihisia kwenye ngoma hiyo na ikapelekea kukutana naye na kufanya kazi ya kihitosria ambayo ni Essence