SINGIDA BLACK STARS WAILALAMIKIA YANGA KUCHUKUA KOCHA WAO…

Muda mfupi baada ya Klabu ya Yanga kumtangaza Kocha wao mpya Hamdi Miloud, Klabu ya Singida Black Stars imesema imepokea taarifa hiyo kwa masikitiko makubwa sababu ya kutofuatwa utaratibu.

Singida Black Stars wameandika ‘Tumepokea kwa mshituko na masikitiko makubwa taarifa ya kocha wetu Hamdi Miloud kutambulishwa na Klabu ya Yanga bila kufuata utaratibu.

Uongozi wa Klabu unalifuatilia jambo hili, tunawaomba mashabiki na wapenzi wa Singida Black Stars wawe watuliv wakati uongozi ukifanyia kazi jambo hili.

Maoni yako ni yapi?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *