Mahakama Kuu ya mjini Lagos imeahirisha kuendelea kusikilizwa kwa kesi ya mwimbaji wa Nigeria Naira Marley, anayeshtakiwa kwa uhalifu wa mtandaoni hadi Novemba 13 na 30.
Hakimu Nicholas Oweibo aliahirisha kesi hiyo siku ya jana, Jumatatu kufuatia kutokuwepo kwa Naira Marley mahakamani.
Shirika la Habari la Nigeria (NAN) limeripoti kuwa Tume ya Uhalifu wa Kiuchumi na Kifedha (EFCC) limemfungulia mashtaka 11, Naira Marley kwa tuhuma za uhalifu wa mtandaoni ikiwemo kufanya ulahai wa fedha.