Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa amewaagiza wakala wa barabara hapa nchini (tanroad) kuacha kutoa kazi nyingine kwa mkandarasi ambae hajafikisha asilimia 60 ya kazi ya awali kwani baadhi ya wakandarasi wamekua wakishindwa kukamilisha kazi kwa wakati kutokana na kua na mrundikano wa kazi.
Bashungwa ameyasema hayo hii leo wakati akiwa katika mkutano wa makandarasi uliofanyika jijini mwanza ambapo amesema kumekua na tabia ya baadhi ya wakandarasi kushika kazi zaidi ya moja huku wakiwa wakiwa hawana vifaa na uwezo wa kusimamia miradi hiyo jambo ambalo limekua kero kubwa sana kwa serikali.
Bashungwa amesema moja ya mradi alioutembelea jijini mwanza ni mradi wa makutano ya barabaya ya Nata-Sanzate unaotekelezwa na Kampuni ya China Railway Seven Group lakini hajaridhishwa na mkandarasi huyo kutokana na utendaji kazi wake kua mdogo hii ni kutokana na kua na miradi zaidi ya minne ambayo anashindwa kuisimamia kwa wakati.
Katika hatua nyingine Bashungwa pia amesema mpaka sasa serikali imeidhinisha kutoa kiasi cha shilingi bilion 70 kwa kila mwezi kwa ajili ya kulipa madeni kwa makandarasi ambapo kiasi cha shilingi bilion 50 kitatolewa kwa ajili ya wakandarasi wa ndani huku lengo la serikali ni kumaliza madeni yote mpaka kufikia November 2023.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Amos makala amewataka wakandarasi wazawa kua makini pale wanapofanya makubaliano ya kazi za ujenzi kwani kumekua na baadhi ya wakandarasi wazawa ambao wamekua wakifanya makubaliano kwa kima cha chini hali ambayo imekua ikiwafanya washindwe kumaliza kazi hizo kwa wakati.