Tani milioni 2 za mbegu ya Pamba kutolewa bure Kishapu – Bashe

Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa amezindua Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mkoani Shinyanga ambapo pamoja na mambo mengine amewaeleza wananchi kuwa katika msimu huu wa kilimo Serikali imetoa takribani kilo Milioni 2 za mbegu zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni mbili katika Wilaya ya Kishapu ambazo zitatolewa bure kwa wakulima ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mfumo wa kutoa ruzuku kwa wakulima wa pamba mkoani Shinyanga.

Waziri Bashe ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa mkoa wa Shinyanga uliofanyika katika kata ya Bubiki, Wilaya ya Kishapu ambapo ametumia pia jukwaa hilo kuzungumza na wakulima wa zao la pamba  ambapo  pamoj ana mambo mengine amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wakulima kwani mpaka sasa wameshatoa trekta 24 kati ya 30 zinazoitajika katika wilaya ya Kishapu ili kurahisisha mazingira ya uzalishaji wa zao la pamba.

“Serikali inafanya jitihada kubwa kuboresha zao la pamba katika Wilaya ya Kishapu kwani mpaka sasa takribaniTani milioni 2 za mbegu ya pamba zenye thamani ya Bilioni 2 zimewafikia wakulima, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mfumo wa kutoa ruzuku kwa wakulima wa pamba” amesema Bashe.

Bashe pia amefafanua kuwa Wilaya ya Kishapu inatarajiwa kupokea dawa za kuulia wadudu/ viwatilifu chupa Milioni 1 vifaa vya kilimo ambapo kila kijiji kitapata trekta 5, na kwamba kila kijiji kwa sasa kitakuwa na Afisa Ugani Kilimo mmoja (1) wa zao la pamba huku akiahidi kwamba kabla ya Uchaguzi Mkuu ujao wa 2025 mtandao wa maji ya Ziwa Viktoria utakuwa umewafikia wanabubiki na Kishapu yote kwa ujumla.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *