Polisi wajipanga kuzuia vurugu kuelekea mwisho wa mwaka

Kuelekea kipindi cha mwisho wa mwaka jeshi la polisi mkoani Shinyanga limejipanga kuimarisha usalama na kuzuia maandamano na mikusanyiko inayoashiria vurugu.

Hayo yamebainishwa leo Octoba 11 2023 na kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Acp . Janeth Magomi wakati wa zoezi la utayari kwa jeshi la polisi mkoani hapa kuelekea mwishoni mwa mwaka.

Akizungumza mara baada ya zoezi hilo lililoambatana na matembezi ya mataa kwa mataa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Acp. Janeth Magomi amebainisha kuwa jeshi la polisi limejipanga kuhakikisha usalama wa wananchi na mali zao na kupiga marufuku maandamano na mikusanyiko inayoashiria vurugu.

Aidha Kamanda Magomi amewataka watumiaji wa vyombo vya usafiri kufuata sheria na taratibu za usalama barabarani lakini pia amepiga marufuku maandamano, mikusanyiko inayoashiria vurugu ndani ya Shinyanga.

Nao baadhi ya wakazi wa Shinyanga wameupongeza mkakati huo ulioandaliwa na jesh la polisi na kuweka wazi kuwa iwapo mkakati huo utatetekelezwa kwa umakini unaweza kutokomeza matendo ya kihalifu ambayo mara nyingi hushamiri katika sikukuu za mwisho wa mwaka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *