Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Wasusia mwili ofisi za bodaboda wakidai rambi rambi

Wasafirishaji Maarufu kama boda boda mkoani Geita wamegoma kumzika mwendesha boda boda mwenzao aliyefahamika kwa jina la Dotto Abeli mkazi wa Nyantorotoro halmashauri ya Mji Geita kwa madai kuwa uongozi wao umekula fedha za rambirambi zinazochangishwa kutoka katika maegesho ya bodaboda mkoani Geita.

Wakizungumza na Jambo Fm waendesha bodaboda hao wamesema wamelazimika kubeba jeneza likiwa na mwili wa marehemu na kulipeleka katika ofisi kuu ya bodaboda iliyopo mtaa wa Misheni mjini Geita kwa lengo la kuwashinikiza viongozi wao kutoa pesa zao wakidai kuna pesa zimepungua zilizopaswa kutolewa kama rambirambi kwenye msibao huo na kuwataka viongozi hao kujiudhulu.

Mwenyekiti wa vijana Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Geita Manjale Magambo amefika katika ofisi hiyo ya bodaboda mkoa wa Geita na kutuliza ghasia hizo huku akitoa kiasi cha shilingi laki tano kumaliza msiba wa mpendwa wao na kuaahidi kikao kikubwa siku ya Jumapili tarehe 1 Oktoba 2023 ili kumaliza changamoto hiyo.

Jeshi la polisi mkoa wa Geita limefika katika eneo la tukio na kuwataka bodaboda hao kuwa watulivu wakati suala lao linashughulikiwa na Jambo FM imefanya Juhudu za kuwatafuta viongozi hao wanaotuhumiwa lakini haijanikiwa na juhudi za kuwatafuta bado zinaendelea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *