EWURA yavifungia vituo vingine viwili vya mafuta

Mamlaka ya udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji Nchini (EWURA) imevifungia Vituo vingine viwili vya Mafuta kwenye Mkoa ya Morogoro na Manyara kwa muda wa miezi sita mara baada ya kujiridhisha pasipo shaka kuwa vituo hivyo vinahodhi mafuta kwa lengo la kupata maslahi binafsi ya kibiashara ikiwemo faida kubwa kinyume na Sheria.

Hayo yamebainishwa leo Septemba 30 2023 Jijini Dodoma na Meneja Mawasiliano na uhusiano EWURA Titus Kaguo wakati akitoa Taarifa kwa Waandishi wa Habari kuhusu muendelezo wa uchunguzi wa Vituo vingine ikiwemo kuwapa fursa ya kuwasilisha utetezi wao ndani ya siku21.

EWURA imewataka Wafanyabiashara wa mafuta pamoja na wamiliki wa vituo vya mafuta kufuata Sheria huku akiwapa onyo kuwa serikali inafuatilia suala hilo kwa karibu na ikithibitika watachukuliwa hatua kali ikiwemo kuwafutia leseni zao.

Katika hatua nyingine Kaguo amesema kuwa Hali ya upatikanaji wa Mafuta ni nzuri lakini bei ya Mafuta katika Soko la Dunia ambayo inasababisha uwezekano wa kupanda kwa bei ya Mafuta kwenye soko la Ndani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *