Orodha ya watu ambao Zoleka Mandela hakutaka kwenye mazishi yake

Septemba 25,mjukuu wa Nelson Mandela, Zoleka Mandela alifariki Dunia na kabla ya umauti kumkuta mwanamama huyo aliweka orodha ya watu ambao hakutaka kuwaona kwenye mazishi yake.

Katika dayari yake,Zoleka aliorodhesha watu ambao hakutaka wahudhurie kwenye mazishi yake ambao ni Thierry Bashala,(Mume wake wa zamani na baba wa watoto wake wawili),Leeroy Andie Cana, (Mume wake wa zamani baba ya mtoto mmoja),pia aliorodhesha baadhi ya watu kutoka familia ya Mandela na Madikizela; Zenani Mandela Snr, Mandla Mandela, Zukiswa Madikizela, Nsundu Madikizela, na Buyelekhaya Dalindyebo.

Zoleka alifariki baada ya kuugua saratani ya metastatic ambayo ilienea kwenye nyonga, ini, mapafu, ubongo, na uti wa mgongo kwa muda wa miaka 11. Marehemu amezikwa siku ya jana Ijumaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *