
Polisi wa Las Vegas nchini Marekani wanamshikilia mwanaume aitwaye Duane “Keffe D” Davis anayeshukiwa kumuua Tupac Shakur kwa kumpiga risasi katika shambulizi lililofanyika nchini humo kwenye gari mwaka 1996, vyanzo vya habari vinasema.
Mwanaume huyo amekamatwa mapema Ijumaa asubuhi, ingawa shitaka hilo halikuwa wazi mara moja, kulingana na maafisa wawili walio na ufahamu wa moja kwa moja wa kukamatwa kwa mtu huyo.