Watu 800 wafariki kwenye tetemeko nchini Morocco

Zaidi ya watu 800 wamefariki dunia baada ya tetemeko la ardhi kutokea nchini Morocco usiku wa kuamkia leo, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi hiyo imesema Watu wengine zaidi ya 600 wamejeruhiwa katika janga hilo.

Tetemeko hilo kubwa lisilo la kawaida limesababisha uharibifu wa majengo katika Vijiji vya milima ya Atlas hadi kwenye Mji wa kihistoria, Marrakech.

Wengi wa waliofariki ni kutoka katika Mikoa mitano iliyo karibu na eneo lililoathiriwa zaidi na tetemeko hilo, idadi ya vifo na majeruhi inatajwa kuwa huenda ikaongezeka wakati waokoaji wakifukua vifusi vya majengo yaliyoanguka na wakijaribu kuyafikia maeneo yasiyofikika kwa urahisi.

Nyumba kadhaa zimeanguka na huduma za umeme hazipatikani huku baadhi ya barabara pia zikiwa hazifanyi kazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *