Wabunge wagomea Trevor Noah kulipwa Bil.4.2 kwa video fupi

Wabunge wa Afrika Kusini wagomea Mtangazaji Trevor Noah, kulipwa kiasi cha  Randi Milioni 33 sawa na takriban Tsh. Bilioni 4.2 kwa Video ya Dakika 5 ili kuitangaza nchi hiyo kama Kivutio cha Kitalii,

Akitoa pendekezo hilo, Waziri wa Utalii, Patricia de Lille amesema kuwa Mcheshi na Mtangazaji huyo atalipwa na Baraza la Biashara la Utalii nchini humo na sio kwa fedha za Umma, ila alijkikuta akipata mpasuko baada ya baadhi ya Wabunge na Wananchi kupinga kwa kudai kuwa Nchi hiyo inapitia Mgogoro mkubwa wa kifedha kwa wakati huu.

Ikumbukwe mchekeshaji huyo ana Asili ya Afrika Kusini na alizaliwa nchini humo mwaka 1984  mjini -Johannesburg,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *