Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

80% Wanawake wanakufa kwa saratani

Imeelezwa kuwa zaidi ya asilimia 80 ya wanawake wanaougua ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi hufariki hapa nchini kutokana na kutokua na uelewa pamoja na kutokujua viashiria vya ugonjwa huo.

Hayo yameelezwa na daktari wa magonjwa ya kina mama kutoka hospitali ya kanda Bugando Dk Amina Jumanne ambae amesema kwa kila wanawake laki moja wanawake 57 ni ambao wanasumbuliwa na ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi na kwa hospitali ya Bugando kwa kila siku wanawake watano hugunduliwa kuwa na maambukizi ya ugonjwa huo.

Dk Amina amesema ugonjwa huo huambukizwa kwa njia ya kujamiana hivyo kwa mwanamke yoyote ambaye tayari ameshafanya tendo la ndoa ana asilimia 80 ya kuwa na maambukizi hayo na viashiria vya ugonjwa huo vinaweza kuanza kujionyesha ndani ya miaka 10 au 20 baada ya kushiriki tendo hilo.

Aidha dk Amina ameongeza kua kundi la watu wenye virusi vya ukimwi, watu ambao wamejifungua watoto zaidi ya wanne na watu ambao hushiriki tendo la ndoa mara kwa mara wapo katika hatari ya kupata ugonjwa huo na amewaomba wanawake wote wenye umri wa zaidi ya miaka 25 ambao tayari wameshiriki tendo hilo kufanya uchunguzi wa mara kwa mara ili kujua hali ya ugonjwa huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *