Klabu ya soka ya Yanga inatupwa nje kwenye michuono ya Ligi ya Mabingwa baada ya kukubali kupigwa penati 3:2 dhidi ya Mamelodi Sundowns.
Hatua ya penati imekuja baada ya kutoka bila kufungana kuanzia Mchezo wa kwanza na huu wa leo wa marudiano.
Katika kipindi cha pili cha Mchezo yanga waliweza kupiga shuti kali kutoka kwa Aziz Ki ila kutokana na VAR shuti hilo ambalo liligonga mwamba halikuwa limeingia golini.