Wifi apandishwa mahakamani kwa kumuua mke wa kaka yake

Elizabeth Josephat (35) Mkazi wa Dar es salaam, pamoja na Faida Daud Masaba (24), Mkazi wa Igoma jijini Mwanza wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Ilemela mkoani mwanza na kusomewa shtaka la mauaji.

Washtakiwa hao wamesomewa shtaka hilo katika Kesi ya Jinai namba 40349/2023 ambapo wote kwa pamoja wanadaiwa kushirikiana kumuua, Flora Philimon Bibwa kinyume na Kifungu namba 196 na 197 ya Sheria ya Kanuni ya Adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2022.

Akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilemela, Fortunatus Kubaja, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Monica Mweli amesema washtakiwa walitenda kosa hilo Novemba 13,2023, eneo la Nyamhongoro wilayani Ilemela mkoani Mwanza.

Baada ya kusomewa shtaka hilo, washitakiwa hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka kisheria ya kusikiliza kesi hiyo na shauri hilo limeahirishwa hadi Januari 4, mwaka 2024.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *