Mvua kubwa iliyoambatana na radi imesababisha vifo vya watu wanne akiwemo mwanafunzi wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Itaba, Eslom Nathan (12) huku wengine nane wakijeruhiwa katika wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma.
Kamanda wa Polisi mkoani humo, Philimoni Makungu amethibitisha kutokea tukio hilo, huku akisema lililotokea saa 1:30 usiku Disemba 19,2023 katika Kijiji cha Buyezi.
Waliofariki ni Vitus Matalo (26), Phita Meshack (36), Fazol Meshack (46) na mwanafunzi wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Itaba, Eslom Nathan (12).