Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

VIDEO: Abaka mtoto wa mwaka mmoja kisa utajiri

Mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Mabula Maduhu mwenye umri wa miaka 23 mkazi wa kijiji cha shinyanga A Wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kumbaka mtoto wake mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu baada ya kushawishiwa na mganga wa kienyeji kuwa akibaka atafanikiwa kwenye shughuli zake za uchimbaji.

Akizungunza na Jambo Fm ofisini kwake kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Geita Kamishina Msaidizi wa Polisi Safia Jongo amesema baada ya kupata ushawishi huo kutoka kwa mganga Mabula alirudi nyumbani na kumkuta mke wake akiwa na mtoto ndipo akamtuma mkewe sokoni na kufanikiwa kumbaka mtoto huyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *