Wenye uchumi wa chini wanaongoza kuwa na watoto wengi

Taarifa ya Uzazi na visababishi vyake kutoka kwenye ripoti ya Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria ya 2022, Utafiti umeonesha kuwa wanawake nchini Tanzania wanazaa wastani wa watoto 4.8.

Kwa ujumla kiwango cha uzazi kimepungua kutoka wastani wa watoto 6.2 mwaka 1991-92 hadi watoto 4.8 kwa mwanamke mwaka 2022.

Wanawake wanaoishi katika maeneo ya vijijini wana uwezo wa kuwa na watoto wengi kuliko wanawake wa maeneo ya mijini (wastani wa watoto 5.5 dhidi ya 3.6 mtawalia).

Kimkoa, uzazi unatofautiana kutoka wastani wa watoto 2.8 kwa mwanamke katika mkoa wa Dar es Salaam hadi wastani wa watoto 6.6 kwa mkoa wa Simiyu.

Kiwango cha uzazi nchini Tanzania kinapungua kulingana na ongezeko la kiwango cha elimu, kutoka wastani wa watoto 6.3 kwa wanawake ambao hawana elimu hadi wastani wa watoto 3.8 kwa wanawake wenye elimu ya sekondari na zaidi.

Aidha, utafiti huu umeonesha kuwa kiwango cha uzazi kinapungua kadiri hali ya uchumi wa kaya unavyoongezeka huku Wanawake wanaoishi kwenye kaya za uchumi wa chini wana wastani wa watoto 6.7 ikilinganishwa na wanawake kutoka kwenye kaya zenye uchumi wa juu (wastani wa watoto 3.3).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *