Watanzania waliotekwa Israel watambuliwa

Serikali ya Israel imethibitisha utambulisho wa Watanzania wawili wanaosadikiwa kushikiliwa mateka na kundi la Hamas tangu Oktoba 7 mwaka huu baada ya kundi hilo la wanamgambo kufanya mashambulio nchini Israel kupitia Gaza.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Israel imewataja Watanzania wanaoshikiliwa mateka na kundi la Hamas kuwa ni Joshua Loitu Mollel na Clemence Felix Mtenga.

Joshua Loitu Mollel na Clemence Felix Mtenga ni miongoni mwa Watanzania wanaosoma mafunzo ya kilimo kwa vitendo nchini Israel na walikamatwa na watu wanaoelezewa kama magaidi wa kundi la Hamas na wanashikiliwa mjini Gaza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *