Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Wenye changamoto ya kusikia na kuona wapewe kipaumbele

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda ameagiza kuwapa kipaumbele wanafunzi wenye changamoto mbalimbali ikiwemo viziwi na wenye uoni hafifu kuwapatia vitendea kazi vinavyoendana na hali zao pamoja na kuacha tabia ya kuwaficha ndani kwa kuwa serikali ipo tayari kuhakikisha wanatimiza ndoto zao.

Profesa Mkenda amesema hayo mkoani Dar es Salaam wakati wa kufungua maonesho ya NECTA, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa baraza hilo.

Aidha Mkenda amesema wataendelea kufanya kampeni ya kuelimisha mabinti wote ili kuendelea kujilinda kiadilifu sambasamba na kusisitiza kuwapa nafasi ya elimu pindi inapotokea wanapata ujazito wakiwa shuleni pamoja na kuwasihi watanzania kuendelea kupinga wizi wa mitihani kwa kuwa si haki, weledi na uadilifu na kutaka shule kushindanishwa pasi na wizi huo wa mitihani.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) Dokta Said ally Mohammed amesema maboresho yaliyosisitizwa na sera ya elimu ya mwaka 2014 iliyoboreshwa toleo la 2023 pamoja na mtaala mpya imesisitiza kuwa na mfumo wa elimu ambao utawezesha kuandaa wahitimu mahiri na wenye ustadi huku akiendelea kusisitiza kuwa necta itaeendelea kuboresha utahini huo ili upimaji uendane na sera hiyo ya elimu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *