Mahabusu alawitiwa Gerezani

Kijana mmoja wa kiume anayeshikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kufanya ulawiti na yeye amenaswa na tuhuma za kufanyiwa ulawiti akiwa mahabusu ya Polisi na Mahabusu mwenzake mwenye umri wa miaka 40.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini magharib Unguja Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Richard Thadei Mchomvu ameeleza hayo mbele ya waandishi wa habari huko Mwembe madema Mjini Unguja wakati waandishi walipotaka kufahamu juu muendelezo wa watuhumiwa wa ulawiti waliotajwa wiki iliyopita na kushikiliwa na Jeshi hilo.

Kamanda Thadei Amesema kikawaida askari polisi hufanya doria kila baada ya saa moja katika mahabusu hizo lakini kitendo hicho kimeripotiwa na mmoja ya mahabusu aliyekuwemo ndani ya kituo hicho na kuita askari na kudai kuwa mahabusu mmoja anamlawiti mahabusu mwenzake.

Aidha amesema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa kesi hiyo ili kuongeza shtaka dhidi yao juu ya makosa waliyoyafanya kwa nyakati tofauti

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *