Wanafunzi hatarini kusombwa na maji Simiyu

Wanafunzi zaidi ya 200 wa shule ya sekondari Simiyu iliyopo kata ya Malambo wilayani Bariadi Mkoani Simiyu, ambao wanaishi katika mitaa ya Matale na Ngashanda, wapo hatarini kusombwa na maji ya mito kutokana na changamoto ya ukosefu wa madaraja katika mito ya Senani na Ndoba ambayo ni lazima waivuke ili kufika shuleni hapo.

Jambo FM imezungumza na baadhi ya wanafunzi hao na hapa wanaeleza adha wanazokutana nazo wakati wa kuvuka mito hiyo kwenda shuleni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *