Na Eunice Kanumba – Shinyanga.
Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimali Watu, David Lyamongi amewataka wazazi na walezi kuwekeza kwa dhati katika malezi na makuzi ya watoto kuanzia wakiwa tumboni ilikuimarisha maadilina kuleta tija kwa taifa katika siku zijazo.
Lyatonga ametoa wito huo wakati akifungua kongamano la maadhimisho ya siku ya kimataifa ya familia kwa mkoa wa Shinyanga kwa niaba ya katibu tawala mkoa wa Shinyanga lililofanyika katika ukumbi wa kalinjuna uliopo katika ofisi ya mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali na serikali wakiongozwa na mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dr Yudas Ndugulile.

Viongozi wengine ni kutoka katika madhehebu ya dini,kamati ya Amani ya mkoa,wawakilishi wa baraza la wazee,baraza la watoto,vyama vya watu wenye ulemavu wadau wa maendeleo,shirika la ICS,klabu ya waandishi wa habari,watalamu wa masuala ya kijamii wanafunzi kutoka vyuo na shule za sekondari ambapo kauli mbiu katika maadhimisho hayo kwa mwaka 2025 ikisema “mtoto na malezi msingi wa familia bora na taifa imara”
“Niwatakie wazazi na walezi wote mkoani Shinyanga kuhakikisha wanawekeza ipasavyo katika malezi na makuzi ya watoto wetu kuanzia wakiwa tumboni ili tuweze kujenga taifa lenye msingi imara maadili na maendeleo endelevu”amesema Lyamongi.

Awali akimkaribisha mgeni rasimi mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dr Yudas Ndugile kongamano hilo lina lengo la kuwaleta pamoja wadau wote wa malezi ya watoto kwa ajili ya kutafakari na kubadilishana uzoefu juu ya jitihada zinazofanywa katika kuimarisha malezi na makuzi bora kwa watoto.
Kwa upande wake afisa ustawi wa jamii mkoa wa Shinyanga Lyidia Kwesigabo amebainisha kuwa kila mwaka may 15 Taanzania huungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha siku kimataifa ya familia ikiwa ni fursa ya kutathimini mchango wa jamii katika maendeleoya watoto na familia kwa ujumla.
