Klabu ya Soka ya Mtibwa Sugar ya Mkoani Morogoro, ambayo imepanda daraja hadi ligi kuu, rasmi imekabidhiwa kombe la ubingwa wa ligi ya NBC Championship kutoka kwa mdhamini mkuu, Benki ya NBC.
Kombe hilo, limekabidhiwa mara baada ya kumalizika kwa mtanange wao wa mwisho uliomalizika kwa sare pacha ya 2-2 dhidi ya Mbeya City ambayo nayo imepanda hadi ligi Kuu ya NBC msimu ujao.
