Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Wauguzi waliotoa kauli chafu kwa mgonjwa matatani

Wizara ya Afya imekemea vikali vitendo vya utoaji wa kauli zisizo za staha na unyanyapaa kutoka Kwa watoa huduma za Afya.

Taarifa Iiliyotolewa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Englibert Kayombo kwenye vyombo vya habari imesema, Wizara hiyo imeeleza kusikitishwa na ujumbe unaosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha mteja anayepata huduma katika kliniki za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (CTC) akilalamika kuhusu kauli zisizo na staha na kunyanyaswa na watoa huduma za Afya wa CTC.

Aidha wizara hiyo imesema itafanya uchunguzi wa tuhuma hizo na watakaobainika kufanya vitendo hivyo taratibu za uwajibishwaji zitafuata kwani vitendo hivyo vinazorotesha utoaji wa huduma bora za matibabu.

Pamoja na mambo mengine Wizara pia imewakumbusha watumishi wa sekta ya Afya kuzingatia maadili ya taaluma zao na kutoa huduma bora za matibabu zenye staha zenye kujali utu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *