Katibu wa NEC siasa Itikadi na Mafunzo wa CCM Paul Makonda amempa miezi 3 waziri wa Tamisemi Muhammed Nchengerwa kuanza mkakati wa kujenga stand ya kisasa Bukoba mjini.
Makonda amempigia simu Waziri Nchengerwa na kumpa maagizo 3 muhimu ya kujenga stand, solo pamoja na kingo za mti Kanoni.
Kwa upande wake Waziri Nchengerwa amesema kuwa amepokea maagizo hayo na watatuma wataalamu kwa ajili ya kuanza kutekeleza maelekezo yake.
Nchengerwa amewaahidi wakazi wa Kagera kwamba atafika mkoani hapo mwezi Disemba kwa ajili ya kuanza kushughulikia mipango hiyo.