Wafanyakazi 13 wa Shania Twain, ambao wapo kwenye tour yake wamelazwa hospitalini tangu siku ya Jumatano, baada ya kupata ajali walipokuwa safarini kuelekea nchini Canada kwenye shoo ya msanii huyo iitwayo ‘Queen Of Me’.
Chanzo cha ajali hiyo kinatajwa kuwa ni hali mbaya ya hewa, na Twain yupo salama, kwani hakuwepo kwenye ajali hiyo.