Jambo La Leo

Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Watoto wa Mr. Ibu wakamatwa kwa kuiba michango

Polisi nchini Nigeria wamewakamata watoto wa mwigizaji wa vichekesho nchini Nigeria John Okafor, maarufu kama Mr Ibu, kwa madai ya kuiba pesa zilizokuwa zikichangishwa kwaajili ya matibabu ya mwigizaji huyo.

Onyeabuchi Okafo na Jasmine Okekeagwu wanadaiwa “kumiliki simu ya mwigizaji huyo na kuingia katika mfumo wa benki”, kabla ya kuiba Naira milioni 55 sawa na dola $60,700 ambazo ni sawa na Tsh. 152,660,501.58.

Pesa hizo ni sehemu ya fedha ambazo zilikuwa zikichangwa na mashabiki na watu wenye mapenzi mema kwa ajili ya matibabu ya mwigizaji huyo, baada ya kuugua kwa muda mrefu mwaka jana.

Ugonjwa huo ulisababisha kukatwa kwa mguu mmoja wa Okafor.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *