Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

VIDEO:Watendaji waliokula hela Geita, moto umewaka

Mkuu wa Wilaya ya Geita Cornel Magembe, amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita kuwarejesha baadhi ya Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji waliohamishwa katika vituo vyao vya kazi vya awali kwa tuhuma za kuondoka na fedha walizokuwa wakichangisha kwa wananchi kwenye maeneo yao bila ya makabidhiano ya kimaandishi na watendaji wapya katika Ofisi zao.

Magembe ametoa agizo hilo katika kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Geita, baada ya kuwepo kwa tuhuma za baadhi ya maafisa kuhama na fedha walizochangisha kwa ajili ya shughuli za maendeleo ikiwemo ujenzi wa Shule na Zahanati.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Charles Kazungu amesema baraza la madiwani tayari wameshamuelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuhakikisha anawaandikia barua watendaji hao ili kurudi kwenye vituo vyao vya kazi vya awali kwa lengo lakuja kurudisha pesa hizo na wakishindwa kufanya hivyo kanuni na taratibu za utumishi zitatumika.

Nao baadhi ya madiwani wa halmashauri hiyo wamesema ni vyema watendaji wanapopata uhamisho kutoka sehemu moja kwenda nyingine wanatakiwa kukabidhi ofisi kwa watendaji wapya kwa njia ya maadishi na wanapo hama na pesa za wananchi wanakwamisha maendeleo katika maeneo hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *