Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Jumuiya za Kimataifa zisaidie kukuza uchumi

Serikali imezitaka Jumuiya za Kimataifa zisaidie kukuza uchumi wa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania ili kupanua wigo wa ushiriki wa wananchi wake.

Hayo yamesema leo Ijumaa, Novemba 17, 2023 na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akiwasilisha tamko la Serikali kwenye ufunguzi wa mkutano wa pili wa Jukwaa la Sauti za Nchi Zinazoendelea uliofanyika kwa njia ya mtandao chini ya uenyekiti wa Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi.

Akizungumza kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Majaliwa ameliomba jukwaa hilo liangalie namna linavyoweza kushirikisha uchumi wa dunia na kuufungamanisha na uchumi wa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania.

Akielezea kuhusu masuala mengine, Waziri Mkuu ameliomba jukwaa hilo lihakikishe linatafuta majibu ya changamoto za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, masuala ya nishati mbadala, uwezeshaji wa vijana na wanawake Jukwaa hilo linaziwezesha nchi zinazoendelea kujadili changamoto zinazowakabili na kupaza sauti zao ili ziweze kuwasilishwa kwenye mkutano wa kundi la nchi 20 zenye maendeleo makubwa ya kiuchumi (G20) utakaofanyika Novemba 20, mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *