Kibu, Inonga, Diarra watozwa faini

Baada ya kufunga bao pekee la klabu ya Simba katika mchezo huo, mchezaji
Kibu Denis alitenda kosa la kwenda kushangilia mbele ya jukwaa la mashabiki
wa Yanga kwa kuonesha ishara ya kuwafunga mdomo.


Kamati imemtoza faini ya Sh. 500,000 (laki tano) mchezaji Kibu Denis kwa
mujibu wa Kanuni ya 17:(14 & 60) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.


Kamati imemtoza faini ya Sh. 500,000 (laki tano) mchezaji Henock Inonga wa
klabu ya Simba kwa kosa la kwenda kushangilia bao mbele ya maafisa wa
benchi la ufundi la klabu ya Yanga.


Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni ya 17:(14 & 60) ya Ligi Kuu kuhusu
Taratibu za Mchezo.


Kocha msaidizi wa klabu ya Yanga, Moussa Ndao ameadhibiwa kwa kutozwa
faini ya Sh. 500,000 (laki tano) kwa kosa la kuwatolea lugha ya matusi maafisa
wa benchi la Ufundi la klabu ya Simba wakati mchezo ukiendelea pamoja na
mchezaji Henock Inonga (wakati wa mapunziko).

Kocha huyo alianza kutoa lugha ya matusi baada ya mchezaji Henock Inonga kwenda kushangilia mbele ya benchi la ufundi la klabu ya Yanga.


Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni ya 17:(14 & 60) ya Ligi Kuu kuhusu
Taratibu za Mchezo.


Kamati imemtoza faini ya Sh. 500,000 (laki tano) mchezaji Djigui Diarra wa
klabu ya Yanga kwa kosa la kwenda kushangilia mbele ya benchi la ufundi la
klabu ya Simba, baada ya timu yake kufunga moja ya mabao yake katika
mchezo tajwa hapo juu.


Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni ya 17:(14 & 60) ya Ligi Kuu kuhusu
Taratibu za Mchezo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *