Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Sabaya ashinda Rufaa, Yupo Huru

Mahakama ya Rufaa imemuachia huru aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai, Kilimanjaro Lengai ole Sabaya na wenzake wawili Sylvester Nyegu na Daniel Mbura baada ya mahakama hiyo kukubaliana na maamuzi ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.

Rufaa hiyo namba 231 ya mwaka 2022 ilikatwa na mwendesha mashtaka wa serikali (DPP) kupinga uamuzi wa awali wa hukumu ya rufaa namba 129 ya mwaka 2021 iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha mbele ya Jaji Sedekia Kisanya iliyompa ushindi Sabaya na wenzake baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 gerezani kufuatia kesi ya jinai namba 105 ya mwaka 2021 iliyohusisha wizi na makundi ya unyang’ayi wa kutumia silaha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *