Wanawake katika Mkoani Shinyanga wamempongeza Rais wa jamuhuri ya Muungano Tanzania Dkt @samia_suluhu_hassan kwa kuwezesha miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta za afya, elimu, miundo mbinu, na maji.
Wakizungumza katika kongamano la kumpongeza Rais kwa mambo makubwa anayoyafanya kwa wanashinyanga lililoandaliwa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, baadhi ya wanawake kutoka katika wilaya mbalimbali za mkoa wa Shinyanga wamesema serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kutekeleza ilani ya chama cha CCM ya mwaka 2020/2025 kwa weledi mkubwa na maendeleo yanaonekana katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Shinyanga.
Awali akizungumza katika hotuba ya ufunguzi wa kongamano hilo mkuu wa mkoa wa Shinyanga Christine Mndeme amesema tangu raisi samia aingie madarakani mwaka 2021 ametoa jumla ya shilingi trilioni moja kwa mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya miradi ya maendeleo na uendeshaji wa shughuli mbalimbali za serikali. Rais dr Samia Suluhu Hassan ni mwenyekiti wa chama wa CCM taifa na aliingia madarakani March 19 mwaka 2021 baada ya kifo cha aliyekuwa rais wa awamu ya tano hayati Dr John Pombe Magufuli huku jamii za kimataifa zikiendelea kumpongeza kwa uwezo mkubwa aliounyesha hususan katika masuala ya diplomasia.