Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Wanafunzi zaidi ya 300 wanatumia chumba kimoja cha darasa

Zaidi ya wanafunzi elfu tatu wa shule ya msingi Tambukareli iliyopo katika wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza wapo hatarini kuathirika kitaaluma kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa uliopo katika shule hiyo kwani kwa sasa chumba kimoja cha darasa kinakaa zaidi ya wanafunzi 300.

Wakizungumzia changamoto hiyo baadhi ya wananchi wa mtaa wa Kanyerere wameiomba serikali iweze kuwapa msaada wa fedha ili waweze kukamilisha vyumba 16 vya madarasa vinavyojengwa kwa nguvu ya wananchi.

Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Kanyerere Kansola Magesa amesema mpaka sasa jumla ya vyumba 16 vya madarasa vimefikia katika hatua ya msingi na wanahitaji kiasi cha shilingi milion miatano kwa ajili ya kukamilisha vyumba hivyo na wanaamini endapo fedha hiyo itapatikana mpaka kufikia mwakani ujenzi wa vyumba hivyo utakua umekamilika na wanafunzi wataanza kutumia madarasa hayo.

Nao baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Tambukareli wamesema wamekuwa wakilazimia kuamka usiku ili kutembea umbali mrefu hali ambayo inahatarisha hali ya usalama wao kwani baadhi yao wamekua wakikutana na wanyama wakali

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *