Staa wa muziki kutoka Nigeria, Tems ameweka wazi kuvutiwa zaidi kisanii na wasanii wawili tu ambao ni Asake, na Tyla kwa hapa barani Afrika.
Tems amesema hayo kupitia Time100 Next Gala huko New York hivi karibuni.
Mtangazaji “Ni wasanii gani wa Kiafrika unaowapenda sasa hivi?”
Tems alijibu: “Wasanii ninaowapenda sana wa Afrika kwa sasa ni Asake na Tyla.”



