Wanafunzi Kidato cha kwanza hadi cha nne kuchagua masomo sasa

Mpango wa wanafunzi kuchangua aina ya masomo na fani wazipendazo na zile ambazo wanauwezo nazo utaanza kwa wanafunzi wanaojiunga kidato cha kwanza hadi kidato cha nne.

Kwa mujibu wa rasimu inayopendekezwa ya Mtaala mpya wa Elimu ya mwaka 2023, wanafunzi watachagua masomo katika moja ya michepuo kulingana na matakwa, uwezo na malengo yao ya maisha. Kwa sasa wanafunzi hulazimika kusoma masomo yote kuanzia kidato cha kwanza hadi cha pili na kuchagua mchepuo wanapoingia kidato cha tatu. Uchaguzi huo ni kwa mkondo wa Elimu ya Jumla na ile ya mkondo wa Elimu ya Amali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *