Afarah suleiman, Babati – Manyara.
Mkuu wa mkoa wa Manyara, Queen Sendiga hii leo Aprili 19. 2025 amezungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake na kuwataka viongozi wa dini kuhubiri amani kwenye nyumba za ibada.
Akitoa salamu za kheri ya Pasaka kwa wakristo wote mkoani humo, Sendiga amesema ni kipindi muhimu cha kutafakari juu ya imani, msamaha na upendo wa kweli nakuwatakia wakristo maadhimisho yenye furaha na baraka.

Aidha, Sendiga amesisitiza viongozi wa dini kulikumbuka Taifa katika sala na maombi, hasa kipindi hiki tunapoelekea uchaguzi mkuu, akisema maombi yao ni muhimu katika kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa utulivu na amani.


