Burna Boy amesema kuwa waandaji wa Tuzo za Grammy ‘Recording Academy’ wameongeza kipengele cha “Best African Music Performance” mwezi Juni, kwenye tuzo hizo kubwa kwa sababu yake.
Staa huyo ambaye ni mshindi wa tuzo ya Grammy 2020 kama ‘Best Global Music Album’ kupitia albamu yake ya ‘Twice As Tall’ amesema hayo kwenye mahojiano aliyofanya hivi karibuni na Los Angeles Times.
“Nina mchango mkubwa kwenye kipengele kipya cha ‘Best African Music Performance’, ambacho ni kizuri, ila Je, ni kipengele kilicholetwa kwaajili ya kuleta faraja?! Na Je!, kitaleta heshima? Nasubiri kuona mwisho wake.”