Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Waita mganga wa kienyeji azindike ili wasihamishwe

Wakazi wa eneo la Kijijini lililopo Kata ya Kawe, Mtaa wa Mbezi Beach B, wamekataa kuhama eneo hilo kama ilivyoelekezwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Matambule aliyetoa Siku 14 (hadi kufikia Novemba 17, 2023) wawe wameondoka kwa hiari yao kwa kuwa eneo hilo ni Hifadhi ya Barabara.

Jeshi la Polisi Wilaya ya Kinondoni, Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini TARURA na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar DAWASA walifika eneo hilo Novemba 17, 2023 na kuwasisitiza wawe wamehama hadi kufikia jana Novemba 19, 2023.

Inadaiwa baadhi ya Wakazi wa hapo wameagiza Mganga wa Kienyeji kutoka Mtwara ili awafanyie zindiko wasiweze kuondolewa.

Hivi karibuni, Mkuu wa Mkoa wa Dar, Albert Chalamila alisema eneo hilo lenye Kaya kati 30-40 limekuwa hatarishi kutokana na uwepo wa watu wengi wanaojihusisha na vitendo viovu ikiwemo uuzaji wa Dawa za Kulevya (Unga), Bangi, Pombe za kienyeji na Biashara ya Ngono.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *