Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Waganga wakuu matatani kifo cha mjamzito

Naibu Waziri wa Afya Dk. Godwin Molel, amewataka Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha wanasimamia ubora wa huduma katika Hospitali na Vituo vya kutolea Huduma za afya na kuhakikisha wanawajengea uwezo watumishi ili kuepuka changamoto na uzembe unaofanywa na baadhi ya wataalamu wa afya nchini.

Dkt. Mollel ametoa agizo hilo leo Novemba 20, 2023 Jijini Dar Es Salaam wakati akizungumza na watumishii wa afya katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke.

Dk. Mollel amesema yanapotokea matatizo katika vituo vya afya alafu Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya hawana taarifa au hawajachukua hatua hadi viongozi wa taifa wanafika watu hao wanatakiwa wajitafakari. Amesema yanapotokea matatizo katika sekta ya afya pamoja na daktari aliyefanya uzembe watu wengine watakao kuwa watuhumiwa ni waganga wakuu wa wilaya na mikoa kwa kutoona na kutatua changamoto kabla hazijatokea.

“Tukija kwenye mkoa wako tukakuta uzembe umetokea mama mjamzito amefariki na Mganga Mkuu wa Wilaya na Mkoa ni mtuhumiwa mpaka vyombo vitakapo chunguza, tukikuta mama, mtoto au mtu yoyote amepata shida alafu mganga mkuu wa mkoa, wilaya na wewe unashangaa inabidi ujitafakari”. Ameeleza Dkt. Mollel.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *