Waandamanaji wamemiminika mitaani kwenye viunga vya mji mkuu wa Israel, Tel Aviv, kupaza sauti za kuikosoa serikali ya waziri mkuu Benjamin Netanyahu na kutoa wito wa kuachiwa huru mateka wanaoshikiliwa na Hamas, Gaza.
Wengi wamebeba mabango makubwa yenye picha za mateka ambao inaaminika bado wanashikiliwa na Hamas ndani ya Ukanda wa Gaza tangu walipokamatwa wakati wa shambulio dhidi ya Israel, Oktoba 7 mwaka jana.
Maandamano hayo yanafuatia mengine makubwa yaliyofanyika mwanzoni mwa mwezi huu mjini Jerusalem katika kile kinachoonekana kuwa migawanyiko miongoni mwa Waisraeli hasa kuhusu namna waziri mkuu Netanyahu anavyoushughulikia mzozo wa nchi hiyo na kundi la Hamas.
Tayari shinikizo linaongezeka la kutaka kuitishwa kwa uchaguzi wa mapema ambao Netanyahu amesema utavuruga kampeni yake ya dhidi ya Hamas na kukwamisha mazungumzo ya kuachiwa kwa mateka.