Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Kenya yasitisha matumizi ya dawa iliyozuiwa  Nigeria

Chombo kinachosimamia usalama wa dawa Kenya, kimeamuru kusitishwa matumizi ya dawa ya maji maji ya kikohozi kwa watoto iliyotengezwa na kampuni ya Johnson&Johhson.

Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Famisia na Sumu (PPB) nchini Kenya imesema imesitisha matumizi na kuamuru kurejeshwa kwa shehena fulani ya dawa ya kikohozi aina ya Benylin Paediatric.


Hatua hii imechukuliwa siku moja baada ya Nigeria kutangaza hatua sawa na hiyo, ikisema dawa hiyo ina kiambata cha sumu ambapo vipimo vya maabara nchini Nigeria vimeonesha dawa hiyo ya maji ina kiwango cha juu cha kiambata kinachoamini kuwa sumu na inauhusishwa na vifo vya watoto kadhaa nchini Gambia, Uzbekistan na Cameroon tangu mwaka 2022.


PPB imesema tayari imeanzisha uchunguzi na inafanya vipimo vyake vya maabara kuthibitisha vile vlivyofanywa na Nigeria. Shehena ya dawa inayolengwa ni ile iliyotengenezwa kampuni ya Johnson &Johnson tawi la Afrika Kusini mnamo mwezi Mei 2021 na kuwa muda wake wa mwisho wa matumizi wa Aprili 2024.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *