Kaimu Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya usaidizi wa kibinadamu(OCHA) Jamie McGoldrick ameeleza kwamba hali ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza imesalia kuwa mbaya licha ya nuru iliyokuwa inaanza kuonekana hivi karibuni baada ya ahadi ya Israeli ya kuongeza msaada.
Amesema kauli ya Israeli ya kwamba malori zaidi ya 1,000 yaliyosheheni misaada yameingia Gaza siku chache zilizopita haina usahihina ukweli ni kwamba malori yaliyoingia upande wa Palestina ni 800 pekee.
Afisa huyo pia amesisitiza kuwa mfumo wa kupeana taarifa baina ya watoa huduma za kiutu kwa kupatiana na pande kinzani kule maeneo waliko ili kuepusha kushambuliwa hadi sasa haufanyi kazi ipasavyo, lakini tayari amewasilisha malalamiko hayo na mengine kwa jeshi la Israeli wakati wa mkutano wao wa kwanza mapema wiki hii.