Watoto wa James Bond , hawatorithi utajiri

Kama unazitaka mali utazipata shambani!!!

Hivyo hivyo pia kwa mwigizaji mkongwe wa Filamu, James Bond ambaye ameweka wazi kuwa hana nia ya kuwapa mali/urithi watoto wake ikitokea amefariki.

James Bond ambaye jina lake halisi ni Daniel Craig, amesema hayo katika mahojiano aliyofanya hivi karibuni.

Utajiri wa Daniel Craig unakadiriwa kufikia dola milioni 160. Hata hivyo watoto zake hawatagusa kitu.

“Si kuna msemo wa zamani kwamba ukifa tajiri, umeshindwa?” alisema katika moja ya mahojiano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *