Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema akiwa Dubai Mashirika mbalimbali yamechangia Tsh. bilioni 2.5 kwa ajili ya kusaidia Waathirika wa janga la mafuriko Hanang.
Akiongea na Wananchi walioathirika na janga hilo katika Shule ya Msingi Katesh Wilayani Hanang leo December 07,2023, Rais Samia amesema “Nawashukuru Watanzania waliotoa msaada kwa njia moja au nyingine, huu ndio upendo tunaozungumza siku zote, janga lilipotokea nilikuwa safarini, taarifa zimetoka wenzetu kule wamesikia na kwahiyo wenzetu kule wengi tu Mashirika yaliyokuwepo kule wametuchangia kiasi cha Tsh. bilioni 2.5 na nimeelekeza waziingize benki”.